Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Kali ya Kufungia Mwaka!! MUME AJINYONGA KWA MTANDIO AKIGOMBEA PESA NA MKE WAKE HUKO KILIMANJARO


Mwanamme aitwaye Elion Mtui (49), mkazi wa  Kijiji cha Masiha,  Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro  amefariki dunia kwa kujinyonga kwa kutumia nguo maarufu kama mtandio kutokana na ugomvi wa kugombea mgao wa fedha kati yake na mkewe.

 Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Geofrey Kamwela,  alisema  tukio hilo lilitokea juzi ambapo  Elion Mtui (49), mkazi wa  Kijiji cha Masiha,  Wilaya ya Moshi,  alijinyonga kwa kutumia nguo maarufu kama mtandio kutokana na ugomvi wa kugombea fedha kati yake na mkewe, Shose Mungu Elion (47).

Kamwela alisema chanzo cha kifo hicho ni baada Sh. 200, 000 zilizotumwa na binti yao, Jesca Elion  kupitia M-pesa ya namba ya simu ya mama yake, hivyo kutokea kutokulewana kuhusu mgao wa fedha hizo.

Alisema muda mfupi baada ya kuzuka ugomvi huo, marehemu Elion alimshambulia mwilini mkewe katika sehemu mbali mbali na kumjeruhi vibaya, tukio  liliwalazimu majirani  kumkimbiza katika Hospitali ya Kitemboni-Marangu na mumewe kuamua kujinyonga.


Bonyeza hapa Tukupe habari zote mara moja zikitoka "HABARI" VITUKO "MAPENZI"MAGAZETI,UDAKU>
Endapo una Habari,Picha,Video,Tangazo au Tatizo Lolote wasiliana nasi kwa namba  +255 688 405 951

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com