KIJANA AUAWA KWA KUCHOMWA MKASI AKIGOMBANIA KOFIA NA MWENZAKE


Polisi wa Lagos, Nigeria wamesema wamemkamata mtuhumiwa Joseph Agwugho kwa tuhuma za kumuua rafiki yake Enya Okpara, kwa kumchoma na mkasi rafiki yake.

Uchunguzi unaonyesha Agwugho na Okpara walikuwa wakigombania kofia ndipo mtuhumiwa alipochukua mkasi na kumchoma nao marehemu shingoni mara tatu.


Okpara alikimbizwa katika Hospitali  Lagos na muda mfupi baadaye kufariki, Agwugho anakabiliwa na kesi ya mauaji, alipandishwa Kizimbani na baadaye kurudishwa gerezani.

Ugomvi wao ulianza kama utani, mmoja hakupendezwa na utani huo, hata alipokasirika mwenzake alidhani utani unaendelea, Agwugho akajikuta akifanya uamuzi ambao ulipelekea rafiki yake kufariki.

Mpenzi Msomaji wetu,Tunapenda kukutumia Habari zetu zote mara tu Tunapoziweka Mtandaoni.Kujiunga nasi Bonyeza Hapa "HABARI" VITUKO "MAPENZI"MAGAZETI,UDAKU>
Endapo una Habari,Picha,Video,Tangazo au Tatizo Lolote wasiliana nasi kwa namba  +255 688 405 951

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post