Raisi wa Zimbabwe Robert Mugabe amewafukuza kazi mawaziri wake wawili na manaibu waziri wapatao watano hatua ambayo imemkumba aliyekuwa makamu wake Joyce Mujuru.
Hatua hii ya kuwafuta kazi mawaziri wake inafuatia hali tete ya kisiasa nchini humo na kujiandaa na lolote litakalotokea lakini pia ni kutokana na mafanikio hafifu ya kiongozi huyo mwenye umri wa miaka tisini endapo atajiuzulu ama kufa.
Mugambe ambaye siku za hivi karibuni ameamua kupumzika katika msimu huu wa sikuku na kuchagua bara la Asia kupumzika yeye na familia yake.lakini wadadisi wa mambo wanasema mafanikio ya Raisi huyo ambayo ni hafifu hayakutarajiwa na walio wengi.
Hofu ya kupokwa madaraka aliyonayo Rais Mugabe ilimsukuma kumtimua kazi makamu raisi wake bi Joyce Mujuru aliyekuwa akipata umaarufu mkubwa kisiasa nchini mwake , na ndipo mkewe bi Grace Mugabe ambaye naye amepanda umaarufu kisiasa na hivyo kumtia Joyce kumshauri afanye hivyo.
Mujuru aliingia katika kashfa ya kutaka kumuua raisi,lakini pia anashutumiwa kukigawa chama cha ZANU PF,na lingine kuonekana kushindwa kwa Mujuru kufunga mikataba ya kibiashara
Kufuatia tuhuma hizo nafasi ya bi Mujuru ilichukuliwa na waziri Emerson Mnangwaga mshirika wa miaka mingi wa raisi Mugabe.
via>>BBC
Endapo una Habari,Picha,Video,Tangazo au Tatizo Lolote wasiliana nasi kwa namba +255 688 405 951