Askofu
wa Kanisa la TFE la mjini Shinyanga, Edson Mwombeki |
Askofu
wa Kanisa la Tanzania Field Evangelism(TFE) maarufu kanisa la Emmanuel la mjini Shinyanga, Edson Mwombeki, amesema
atakipigia ‘debe’ Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), katika
uchaguzi mkuu ujao.
Askofu Mwombeki alitoa ahadi hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita mjini Shinyanga wakati akiwaweka wakfu viongozi wapya wa Chadema walioshinda
katika uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji mbele ya
Mbunge wa Viti Maalum Shinyanga Mjini, Rachel Mashishanga.
Alisema maono aliyoyapata, chama hicho kitakuwa mkombozi kwa Watanzania
katika kuwaletea maendeleo na si chama kingine, hivyo atahakikisha
anakuwa mstari wa mbele kinapata ushindi katika majimbo ya Kishapu na
Shinyanga Mjini.
“Magari yangu mawili yatatumika kufanya kampeni kwa gharama zangu katika
majimbo haya kutokana na kutokuwa na viongozi wazuri na kutozingatia
maslahi ya wananchi,” alisema Mwombeki.
Aidha, alisema CCM iliyoachwa na hayati Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere, siyo CCM ya sasa kwani haina sera nzuri, viongozi wabovu ambao
hawafuati sera ya chama hicho na badala yake wanafuata mambo yao
binafsi.
"Viongozi hasa wabunge waliochaguliwa na wananchi hawako karibu na viongozi wa dini na wananchi wao,hii ni kero kubwa,wabunge badala ya kuwa karibu na wananchi wao sasa wamekuwa walanguzi wa wananchi",alisema Askofu Mwombeki
"Wakati wa uchaguzi wamekuwa wakijidai kutumia pesa zao na kupenda kuwarubuni wananchi katika jamii na walioko makanisani ,hii ni kero,vitendo vyao haviridhishi mfano mbunge anapodiriki kwenda kununua viwanja vya kanisa na kuvifanya kuwa gereji",aliongeza Mwombeki.
Na Mwandishi wa Malunde1 blog-Shinyanga
Endapo una Habari,Picha,Video,Tangazo au Tatizo Lolote wasiliana nasi kwa namba +255 688 405 951