Mwanamke aliyejulikana kwa
jina Ting Su nchini China amemwacha mumewe na dadake bila nguo
barabarani baada ya kuwakuta wakifanya mapenzi.
Ting Ting Su aligundua
kwamba mumewe alikuwa akimsaliti na dadaake ndipo alipoamua kuwafuata hadi katika
kituo kimoja cha maduka akitumia teknolojia katika simu yake ambapo
aliwapata wakichemshana katika gari la mumewe.
Wawili hao
walitoka ndani ya gari hilo bila nguo kwa kubabaika ili kujaribu
kumuelezea kilichokuwa kikiendelea lakini waliachwa na mshangao mkubwa
wakati Ting alipoingia ndani ya gari hilo na kuondoka kwa haraka na
kuwaacha wawili hao barabarani bila nguo.
Kwa mujibu wa
gazeti la Metro,shahidi aliyejulikana kama You Meng alisema
walioshuhudia kisa hicho walibeba simu zao na kuanza kuchukua picha na
yeye hakubakia nyuma.
Mumewe aligonga dirisha la gari hilo na kumpigia kelele mkewe lakini hakujali kamwe aliliondosha gari hilo kwa haraka.
via>>BBC
Social Plugin