MAJAMBAZI YANYONGA MWANAFUNZI KWA KITANDA ALIYEPIGA KELELE YALIPOVAMIA NYUMBA
Monday, December 29, 2014
Watu
wanaosadikiwa kuwa majambazi wamevunja nyumba na kupora mali mbalimbali
kisha kumnyonga mwanafunzi Isihaka Beda wa darasa la saba shule ya
msingi Jitegemee iliyopo makao makuu ya wilaya ya Handeni hatua ambayo
imesababisha majonzi makubwa kwa wakazi wa wilaya hiyo.
Vilio vya wakazi wa wilaya ya Handeni vilitawala kufuatia
watu wasiojulikana kuvunja nyumba ya mkazi mmoja Abida Zubeir wa eneo la
Kivesa lililopo makao makuu ya wilaya ya Handeni ambapo wanadaiwa
kuvunja na kuiba TV, Deki, Godoro na vifaa vingine mbalimbali kisha
kumnyonga mwanafunzi beda kwa kutumia mti wa kitanda cha miti wakati
alipokuwa akipiga mayowe.
Kufuatia hatua hiyo baadhi ya makundi ya wazee na viongozi wa mitaa
wa wilaya ya Handeni wameiomba serikali kuhakikisha wanawatumia baadhi
ya vijana kusaidiana kufichua wahalifu ambao wanaishi nao katika jamii
ili kupunguza kasi ya vitendo vya mauaji ya kutisha yanayotishia usalama
wa wananchi.
Kamanda wa polisi mkoani Tanga naibu kamishna wa jeshi la polisi
Frasser Kashai amethibitisha kutokea kwa tukio na amewaomba wananchi wa
wilaya ya Handeni na mkoa wa Tanga kwa ujumla kutoa ushirikiano kwa
jeshi la polisi ili kuhakikisha kuwa vitendo hivyo vinakomeshwa.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin