Mrembo mmoja amejirusha baharini katika kivuko cha
ferry mapema leo adhuhuri wakati akiwa amepanda kivuko/ferry ya MV Harambee
kutoka upande wa Mombasa Kisiwani kuelekea Likoni.
Msichana huyo mwenye umri kati ya miaka 20 na 25
amejirusha kutoka eneo la juu ya Kivuko wakati fery/kivuko ikiwa katikakati ya bahari ikielekea ufukweni.
Wapiga mbizi wa shirika la Kenya ferry wamejaribu
kuokoa maisha yake baada maji kumzidi kutokana na mawimbi makali na akafanyiwa
huduma ya kwanza na hatimaye kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Likoni.
Kwa
sasa anapokea matibabu katika hospitali moja mjini Mombasa.
Kulingana na afisa wa uhusiano mwema wa shirika la
Kenya Ferry Harun Mutiso amesema kwamba maafisa wa polisi wanachunguza
kilichopelekea msichana huyo kutaka kutoa uhai wake.
Hata hivyo kulingana na walioshuhudia ni kwamba
wanadada huyo alionekana mtulivu na hakuna aliyetarajia kwamba anaweza jirusha
kutoka eneo la juu ya Ferry hadi ndani ya bahari.
Haya yanajiri siku moja baada ya mwanadada mmoja
kutoka mtaa wa Mbuzi huko Likoni kumtumia rafiki yake wa kiume ujumbe mfupi
kutumia simu ya rununu kwamba atajinyonga kutokana na hali ya maisha kuzidi
kuwa ngumu kwake.
via>>http://www.radiorahma.co.ke
Endapo una Habari,Picha,Video,Tangazo au Tatizo Lolote wasiliana nasi kwa namba +255 688 405 951
Social Plugin