Maskini!! MZEE HUYU ACHARANGWA MAPANGA HUKO GEITA

 Seleman Mlela mwenye umri wa miaka 75 mkazi wa Nyarugusu Wilayani Geita Mkoani Geita akiwa anauguza majeraha katika hospitali ya Wilaya Geita baada ya kuvamiwa na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake juzi-Picha  na Valence Robert-Malunde1 blog Geita.

Mkazi mmoja wa kijiji cha Nyarugusu wilayani Geita mkoani Geita Seleman Mlela(75)amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Geita baada ya kunusurika kifo kwa kucharangwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwemo kwenye paji lake la uso.

Tukio hilo limetokea juzi katika kijiji cha Nyarugusu wilayani Geita mkoani Geita 
Akizungumza kwa shida na Malunde1 blog ilipomtembelea katika wodi namba 8 alikolazwa Mlela amedai kuwa siku ya tukio alipigiwa simu na watu wasiofahamika wakimtaka atoe shilingi laki 6 kukomboa ng’ombe zake zilozokuwa zimekamatwa na baada ya kuelekea maeneo aliyoelekezwa hakufanikiwa kuwakuta watu hao na kuamua kurudi nyumbani.

Ameongeza kuwa akiwa hana hili na lile alivamiwa na watu wasiojulikana nyumbani kwake kisha kumkatakata mapanga.

Mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Geita Dk Adam Sijaona aliiambia Malunde1 blog kuwa hali yake inaendelea vizuri ikilinganishwa na hali alivyofikishwa hospitalini hapo.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Geita  Joseph Konyo amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kwamba uchunguzi unaendelea ili kuwabaini na kuwakamata wahusika ili sheria ichukue mkondo wake.

Na Valence Robert-Malunde1 blog-Geita

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post