Ratiba ngumu ya mechi za msimu wa sikukuu za Krismasi na mwaka mpya katika ligi kuu ya Uingereza imeanza rasmi leo.
Chelsea ambao wanaongoza ligi ndio walifungua pazia za mechi za leo
kwa kukipiga na West Ham United katika uwanja wa Stamford Bridge.
Matokeo ya mchezo huo ni ushindi wa magoli mawili kwa bila kwa Chelsea.
John Terry alianza kufungua akaunti ya magoli kwa Chelsea katika
kipindi cha kwanza, kabla ya Diego Costa kuongeza goli la pili kipindi
cha pili na kuhitimisha ushindi huo ambao wamewapa uongozi wa pointi 6
kileleni.
Social Plugin