Mvua
kubwa zilizonyesha kwa muda mfupi mjini Morogoro zimesababisha mafuriko
baadhi ya barabara kushindwa kupitika na maji kujaa katika baadhi ya
maduka.
Wakazi wa mji wa Morogoro wakizungumzia mafuriko hayo wamelalamikia
miundombinu mibovu ya barabara kutokana na kuziba kwa mitaro ambapo
wameitaka halmasauri ya mji wa Morogoro kuzibua mitaro hiyo huku baadhi
ya wafanyabiashara wakilalamikia kupata hasara.
Katika hatua nyingine mto Kikundi uliopo mjini Morogoro umepoteza
uelekeo na kumwaga maji katika soko kuu la mji wa Morogoro na
kusababisha maji kujaa katika maduka huku baadhi ya magari yakiingia
kwenye mitaro na baadhi ya bodaboda zikiwa na abiria zime zama katika
maji na kulazimika kuvutwa.
Kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Morogoro Phimlemon Magesa
akizungumzia alalamiko hayo ya wananchi hao amesema manispaa
wanajitahidi kufanya usafi lakini tatizo liko kwa wananchi wenyewe
kutupa taka kwenye mitaro na kusabisha mitaro hiyo kuziba na maji
kupoteza ueleko na kujaa katika makazi ya wananchi.
via>> itv.co.tz
Endapo una Habari,Picha,Video,Tangazo au Tatizo Lolote wasiliana nasi kwa namba +255 688 405 951