MREMBO WA CHUO AFARIKI DUNIA KWA KULISHWA SUMU,ALIKUWA ANAKULA UJANA USIKU


 Marehemu Neema Malimbwi enzi za uhai wake


WAKATI Wakristo kote nchini wakijiandaa kusherehekea Sikukuu ya Krismasi, keshokutwa Alhamisi, baadhi ya familia zipo kwenye majonzi mazito kufuatia kuondokewa na ndugu zao. 


Jijini Dar es Salaam, binti mbichi aliyejulikana kwa jina la Neema Malimbwi (pichani) ambaye alikuwa mwanafunzi wa Chuo cha Kodi Tanzania (ITA) ambacho kipo chini ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),  kilichopo Mikocheni jijini Dar amefariki dunia kwa madai ya kulishwa sumu kwenye kinywaji.

Marehemu Neema alikuwa binti wa  profesa wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine Morogoro (Sua), Rogers Malimbwi. 

SIKU YA TUKIO
Tukio hilo la kusikitisha linatajwa kutokea usiku wa Alhamisi,  Desemba 18, mwaka huu wakati Neema anarudi hosteli maeneo ya Kijitonyama, Dar ambapo alikuwa akiishi. 



ALIKWENDA KUJIRUSHA B BAND

Kwa mujibu wa chanzo chetu, siku ya tukio, Neema alikuwa na marafiki zake wavulana kwa wasichana kwenye onesho la muziki wa B Band inayomilikiwa na Banana Zorro ambapo akiwa huko saa 7 usiku aliendelea kuchati na marafiki zake waliokuwa hosteli akitumia ukurasa wake wa Facebook akiwaambia kuwa alikuwa ‘kiwanja’ akiponda raha.   
Baba wa marehemu Neema Malimbwi, Prof. Rogers Malimbwi. 


Habari zinadai kuwa, marehemu Neema usiku huo alikuwa akihama maeneo mbalimbali akiwa na vijana ambao baadhi ya marafiki zake wanadai huenda walihusika na kumtilia sumu kwenye bia alizokuwa akinywa. 


MATATIZO YALIPOANZA
Habari zaidi zinasema kuwa, Neema akiwa na wenzake wakirudi hosteli, njiani alianza kulalamikia kutojisikia vizuri.




“Alikuwa njiani na wenzake wakirudi kulala, akaanza kulalamika kwamba hajisikii sawasawa, ikabidi wenzake wamkimbize Hospitali ya Mkoa wa Kitabibu wa Kinondoni, Palestina, Sinza, Dar ambako waliambiwa kuwa kutokana na hali yake kuwa mbaya wampeleke kwanza Kituo cha Polisi cha Kijitonyama ‘Mabatini’ jijini Dar ili kupata hati ya matibabu (PF3),” kilisema chanzo kimoja.Chanzo hicho kikaendelea kudai kwamba, walipofika Mabatini waliambiwa waende Kituo cha Polisi Oysterbay. 

AKIMBIZWA HOSPITALI YA MWANANYAMALA
Ikazidi kudaiwa kuwa, Polisi Oysterbay walitoa msaada kwa haraka ambapo sasa ikabidi Neema akimbizwe Hospitali ya Mkoa wa Kitabibu Kinondoni, Mwananyamala ambako alifariki dunia.



ALIJITABIRIA KIFO

Chanzo hicho kilisema kuwa, denti huyo alikuwa kama anafahamu siku ya kifo chake ambapo siku moja kabla alimshukuru Mungu kupitia ukurasa wake wa Facebook kwa yote aliyomfanyia kisha kutuma picha mbalimbali akiwa katika pozi tofauti. 

MWILI WAKE MOCHWARI
Mwili wa Neema ulihifadhiwa kwenye mochwari ya Mwananyamala kabla ya kusafirishwa juzi kwenda Morogoro kwa mazishi yaliyofanyika jana. 

KUMBUKUMBU MBAYA
Kumbukumbu zilizopo zinaonesha kuwa, Juni Mosi, mwaka jana, mama mzazi wa Neema, Elizabeth Malimbwi alifariki dunia kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar na mwili wake kwenda kuzikwa Morogoro. 

Tangu kifo cha mama yake, baadhi ya madenti wenzake wanasema, Neema amekuwa akiishi maisha ya mawazo sana na muda mwingi alikuwa akiutumia kunywa pombe kiasi kwamba, darasani ilikuwa mara chache sana kuhudhuria.

Neema Malimbwi enzi za uhai wake akiwa hosteli

RPC ATHIBITISHA KIFO

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, ACP Camillius Wambura alikiri kuwa na taarifa hizo.“Ni kweli taarifa za kifo cha mwanafunzi huyo ninazo,  mpaka sasa jeshi la polisi linasubiri ripoti kamili ya uchunguzi wa madaktari kuhusiana na kifo chake,” alisema Kamanda Wambura.


Mpenzi Msomaji,Tunapenda kukutumia Habari zetu zote mara tu Tunapoziweka Mtandaoni.Kujiunga nasi Bonyeza Hapa "HABARI" VITUKO "MAPENZI"MAGAZETI,UDAKU>
Endapo una Habari,Picha,Video,Tangazo au Tatizo Lolote wasiliana nasi kwa namba  +255 688 405 951

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post