Jeshi
la polisi mkoani Shinyanga linamshikilia mkazi wa kijiji cha Kibara
wilayani Bunda mkoani Mara Jonathan Daniel (33) kwa tuhuma za
kupatikana na noti bandia 75, za shilingi elfu kumi kila moja zenye
thamani ya shilingi 750,000, pamoja na vifaa vya kutengenezea pesa hizo
bandia.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na
kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga Bw. Justus Kamugisha amesema tukio
hilo limetokea Desemba 27 mwaka huu,majira ya saa 2 na dakika 45 usiku katika eneo
la kituo cha mabasi kwenye kijiji na kata ya Kakola tafara ya Msalala
wilayani Kahama.
Amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa na askari wa jeshi hilo wakati
wakiwa katika doria ya kawaida kwenye kituo hicho cha mabasi akiwa na
noti hizo bandia na kuwa kati yake noti 3 zina namba BL, 0315207, noti
(32) BB 0315203, noti (21) BE 0315206 , na noti (19) zikiwa na namba BC
0315209.
Kamanda Kamugisha amesema licha ya kumkamata mtuhumiwa na
noti hizo bandia, pia amekamatwa akiwa na bando ya karatasi , Sindano
pamoja na chupa ya konyagi iliyokuwa na unga mweupe, vifaa ambavyo
vinasadikiwa kuwa vinatumika kutengenezea noti hizo.
Aidha kamanda Kamugisha ameongeza kuwa Mtuhumiwa huyo anatarajiwa
kufikishwa mahakamani wakati wowote kujibu tuhuma zinazo mkabili mara
baada ya upelelezi wa jeshi hilo kukamilika.
Social Plugin