Maafisa nchini Marekani wanasema
kuwa mtoto mmoja mdogo mvulana wa miaka miwili amempiga risasi kimakosa
mama yake mzazi na kumuua ndani ya duka moja kubwa la uuzaji bidhaa la
Wal-Mart.
Maafisa wa usalama wanasema bunduki iliyotumika
iliyokuwa imefichwa ilichomoka wakati mvulana huyo alipokaribia na
kuligusa begi la mkononi la mama yake mwenye umri wa miaka 29.
Tukio hilo limetokea katika mji wa Hayden, katika jimbo la Idaho.
Msemaji wa Kaunti hiyo anasema mwanamke huyo alikuwa na kibali cha kumiliki silaha.
Social Plugin