Kama ulifanikiwa kuisherehekea Christmas
ya mwaka huu 2014 kwa amani basi ni heri kwako, kumbe wakati wengine
wakisherekea kwa amani Sikukuu hii kubwa ya mwaka kuna sehemu ambazo
hakukuwa na heri yoyote siku hiyo.
Story hii ya kusikitisha inatoka Kenya ambapo jamaa mmoja Daniel Imonje,
alimpiga mke wake kwa shoka mpaka kufariki, majirani walioshuhudia
wakisema eti kisa ilikuwa ni kitendo cha mke wake huyo kutomuandalia
mume wake nyama ya kuku siku ya Christmas, badala yake akaandaa rosti ya
nyama ya ng’ombe.
Ni wengi waliolaani kitendo hicho
kilichotokea Kijiji cha Shanderema, Kenya na mashuhuda wamesema Daniel
alifanya unyama huo akiwa amelewa.
Mtuhumiwa anashikiliwa katika kituo cha Polisi cha Kakamega baada ya kufanya mauaji hayo kwa ajili ya uchunguzi.
Endapo una Habari,Picha,Video,Tangazo au Tatizo Lolote wasiliana nasi kwa namba +255 688 405 951
Social Plugin