MVUA YALETA KIZAA ZAA KIJIJI CHA TUMBI MANISPAA YA TABORA,KAYA 30 ZAKOSA MAKAZI


Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tabora mjini Bw.Moshi Abrahamu akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa Waathirika wa mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali na kuezua na kubomoa nyumba zaidi ya 23 huku kaya zaidi ya 30 zikikosa makazi katika kijiji cha Tumbi manispaa ya Tabora.
Katika nyumba hii bibi mmoja amenusurika kifo baada ya nyumba yake kuanguka kuta zake tatu kutokana na mvua hiyo iliyonyesha kwa muda wa saa moja kuanzia saa kumi na mbili jioni.


Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tabora mjini akiwafariji baadhi ya waathirika wa maafa hayo ya Mvua katika kijiji cha Tumbi manispaa ya Tabora
Mwenyekiti Moshi Abrahamu kwa kushirikiana na baadhi ya viongozi wa CCM wilaya ya Tabora walilazimika kuchangishna na kupata kiasi kidogo cha fedha kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa maafa hayo ambapo aliwapatia maturubai kama sehemu ya huduma ya kwanza ya hifadhi kutokana na janga hilo.
Viongozi hawa wa CCM wilaya ya Tabora mjini wakimpa pole mmoja wa wakazi wa kijiji cha Tumbi baada ya maafa hayo ya Mvua kubwa.PICHA ZOTE KWA HISANI YA KAPIPIJ BLOG

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post