Mwanafunzi wa darasa la sita katika Shule ya Msingi Kivesa
wilayani Handeni Mkoa wa Tanga, Isiyaka Beda (14) amefariki dunia baada
ya kunyongwa na kuvunjwa shingo na watu wanaodaiwa kuwa ni wezi.
Mama wa marehemu, Abida Zuberi alisema jana kuwa
tukio hilo lilitokea juzi usiku.
Alisema siku hiyo mtoto huyo alikwenda kulala kwenye nyumba ya dada yake ambaye amelazwa hospitali.
Alisema siku hiyo mtoto huyo alikwenda kulala kwenye nyumba ya dada yake ambaye amelazwa hospitali.
Zuberi alisema mwanaye aliombwa na shemeji yake akalale huko kwa kuwa yeye amesafiri kikazi.
Alisema usiku wakati Beda amelala waliingia watu
katika nyumba hiyo yenye vyumba viwili na sebule na kwenda chumbani
alimolala kisha wakamnyonga na kuiba magodoro na runinga na wakatokomea.
Alisema asubuhi yake alipigiwa simu na mkwe wake (mume wa mtoto wake) kuwa amerudi safari ila hali aliyoikuta kwake siyo nzuri.
“Aliniambiwa kuna wezi wamevunja milango na kuiba,
lakini nikamuuliza Beda mzima...Hakutoa jibu la moja kwa moja ndiyo
nikaamua kurudi nyumbani nikamkuta amefariki dunia,” alisema.
“Wezi hao walivunja chumba cha kwanza na baadaye
kuingia alikolala Beda. Mimi nipo hospitali kwa wiki nzima sasa
ninamuuguza mwanangu mwingine,” alisema.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Fraisser Kashai alisema uchunguzi wa kifo hicho bado unaendelea ili kuwabaini waliohusika.
Aliwataka wananchi kutoa taarifa polisi kwa
kuwataja watu wanaodhani kuwa ndiyo wahusika wakuu kwenye masuala ya
uhalifu katika jamii ili sheria ichukue mkondo wake.
Na Rajabu Athumani, Mwananchi
Na Rajabu Athumani, Mwananchi
Endapo una Habari,Picha,Video,Tangazo au Tatizo Lolote wasiliana nasi kwa namba +255 688 405 951
Social Plugin