Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAJASIRIAMALI WAVUNA ZAWADI KIBAO KUTOKA COCA COLA MJINI KAHAMA

Kushoto ni Mwakilishi wa Mama Kelvin shop mjini Kahama akipokea TV  ya flat screen nchi 32 aina ya SONG yenye thamani ya shilingi milioni  moja na laki nane katika droo maalumu ya zawadi kutoka kampuni ya vinywaji Tanzania Cocacola iliyofanyika mjini Kahama -picha na Philipo Chimi-Malunde1 blog Kahama
 
Meneja wa kampuni ya vinywaji  COCACOLA wilaya ya Kahama Machela Chacha,katikati ni meneja mauzo COCACOLA kanda ya Ziwa Nzweke Mussa,kulia ni meneja Cocacola mkoa wa Shinyanga Maximilian Bandoma wakiwakatika droo maalumu ya zawadi kutoka kampuni ya vinywaji Tanzania Cocacola -picha na Philipo Chimi-Malunde1 blog Kahama


Wajasiriamali na wafanyabiashara kutoka Kahama wakiwa wameshikilia vyeti vya ushiriki  katika droo maalumu ya zawadi kutoka kampuni ya vinywaji Tanzania Cocacola-picha na Philipo Chimi-Malunde1 blog Kahama

 Kushoto ni  mmiliki wa Tawifiq Shop mjini Kahama akishikana mkono na viongozi kutoka kampuni ya vinywaji Tanzania Cocacola ambapopia alikabidhiwa kreti 10 za soda-picha na Philipo Chimi-Malunde1 blog Kahama
 Washindi 15  wa kreti 10 za soda kila mmoja katika droo maalumu ya zawadi kutoka kampuni ya vinywaji Tanzania Cocacola-picha na Philipo Chimi-Malunde1 blog Kahama


Zaidi ya wajasiriamali 41 na wafanyabiashara wadogo wilayani Kahama  mkoani Shinyanga wamevuna zawadi mbambali kutoka katika droo maalumu ya zawadi katoka kampuni ya vinywaji Tanzania Cocacola.

Akizungumza katika droo hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Niteshi mjini Kahama meneja mauzo kanda ya ziwa kutoka katika kampuni hiyo Nzweke Mussa amewapongeza wafanya biashara wa soda kutoka kampuni hiyo kuuza bidhaa za kampuni hiyo kwa mwaka mzima na kuiwezesha kampuni hiyo kumudu ushindani wa masoko katika mwaka huu 2014 .

Amesema kutokana na mchango mkubwa wa wafanyabiashara wa soda wilayani humo kununua kwa wingi bidhaa kutoka  katika kampuni hiyo imewezesha kutoa zawadi kwa wateja wao kama fadhira kwa kuwa wadau wao wakubwa wa vinywaji  hivyo kupitia  droo maalumu ya zawadi wametoa kreti 150 kwa wateja 15 ikiwa kila mmoja ameshinda kreti 10 za soda.

Ameongeza kuwa katika droo hiyo  zawadi nyingine kubwa iliyotolewa ni TV  ya flat screen nchi 32 aina ya SONG yenye thamani ya shilingi milioni  moja na laki nane ambapo mshindi mmoja kutoka mjini Kahama Mama Kelvin shop ndiye amejinyakulia zawadi hiyo.

Naye meneja wa Cocacola mkoani Shinyanga Maximillian Bandoma amewapongeza wajasiriamali na wauzaji wa soda za cocacola kwa kuwaunga mkono katika biashara kwa kipindi chote cha mwaka 2014.

Bandoma ameahidi kuwa kampuni hiyo itaendelea kutoa zawadi nyingine nyingi  kubwa kwa mwaka ujao 2015 na kuwaomba waendelee kuwa na ushirikiano na kampuni hiyo.

Kwa upande wao washindi wa zawadi katika droo hiyo akiwemo mshindi wa zawadi ya Flati screen nchi 32 Prisca Madi kutoka Kahama mjini Mama Kelvin shop,na mshindi wa kreti kumi kutoka Nyasubi Yaredi Ezekiel {yared shop}wamesema wamenufaika na zawadi hizo kwani zitaongeza mtaji na kukuza biashara zao na hivyo  kuiomba kampuni ya cocacola iendelea kuwaunga mkono wafanyabiashara hao kwa kutoa ofa za zawdi nyingine kama hizo zilizo tolewa.

Kampuni ya cocacola  imetoa zawadi ya kreti 10 kwa kila mshindi,saa moja ya ukutani,mipira miwili,vuvuzela kumi pamoja na flati screeni aina ya Song nchi 32 ikiwa ni droo ya tatu kufanyika huku droo nyingine tatu zimekwisha fanyika ambapo kreti 75 zilitolewa kwa kila droo.

Katika mwaka 2014 kampuni hiyo imetoa jumla ya kreti 300 kwa wateja wake pamoja na zawadi nyingine ikiwemo trei na glasi.

Na Philipo Chimi-Malunde1 blog Kahama

Bonyeza hapa Tukupe habari zote mara moja zikitoka "HABARI" VITUKO "MAPENZI"MAGAZETI,UDAKU>
Endapo una Habari,Picha,Video,Tangazo au Tatizo Lolote wasiliana nasi kwa namba  +255 688 405 951

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com