PRODUCER MANGU ANUSURIKA KUPATA AJALI SHINYANGA MJINI

Producer wa Diamonds records Mangu Abbas amenusurika kupata ajali baada ya gari lake kutaka kugonga punda waliokuwa barabarani waliokatiza ghafla barabarani katika daraja la Ibinzamata mjini Shinyanga.
Inaelezwa kuwa Producer Mangu alikuwa anatoka Shinyanga mjini kuelekea Standi ya Ibinzamata majira ya saa 8 na dakika 45 usiku akiwa na gari yake aina ya rov 4 ambapo ghafla punda wawili walikatisha barabarani. Akisimulia hali ilivyokuwa Producer Mangu amesema: ""Jamani Wanashimyanga jana ni almanusura nipate ajari katika barabara ya Ibinzamata ambayo ni barabara kuu ya kutoka Dar es salaa kwenda Mwanza ,Chanzo cha yote ni Punda waliozagaa barabarani usiku huo, inaniumiza sana kuona mji wangu niupendao wakazi wake tukiwa sio wastaarabu, tunafuga wanyama na hatuwandalii mazingira na matokeo yake wanasababisha ajari.Na ajari ikitokea utasikia madereva maraaa ooohhh kumbe sababu zingine ni sisi wananchi na tukumbuke usiku ni muda wa mabasi ya Dar kwenda Mwanza yanapita eneo hilo ni hatari sana"
Hata hivyo inaelezwa kuwa mara nyingi wanyama aina ya punda wamekuwa wakionekana katika eneo la Ibinzamata na maeneo mengine mjini Shinyanga

Producer Mangu akiwa kazini


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post