TAZAMA PICHA- HUYU NDIYO MTANGAZAJI NA MWANDISHI WA HABARI MCHAFU KULIKO WOTE DUNIANI


Katika maisha ya kawaida tumezoea kuona kuwa watangazaji na waandishi wa habari hupendelea kuonekana SMART kwani wao ni kioo cha jamii,,ila kwa hili ni tofauti>>>>>
 Pichani ni Raphael Tenthani, mwakilishi wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) nchini Malawi.

Aina yake ya mavazi na uvaaji wake umezua gumzo katika mitandao jamii. Ralph amezoeleka kuonekana katika mavazi ya 'hovyo hovyo', yaliyolowa, machakavu na yaliyotoboka huku viatu vikiwa vimeachama, nywele 'vululu vululu' na sura ya 'kilevi'.

Mwandishi huyu wa habari hujihudhurisha alivyo katika kazi zake mbalimbali za kuhojiana na kurusha habari bila kujali ustaarabu wa eneo husika hata ikiwa ni kwenye zulia jekundu.



Wengi wanasema mkosoaji huyu mkubwa wa Serikali zote zilizoongozwa na Marais ndugu, Bingu (marehemu) na Peter Mutharika, huenda anafanya hivyo ili kutimiza masharti ya 'mganga' aliyemsaidia kupata ujasiri, akili nyingi na kazi katika shirika kubwa la utangazaji la BBC. Wanadai ikiwa atakiuka masharti hayo, huenda akapoteza kazi yake na kuwa 'juha'.

Vyovyote viwavyo, Raphael  "Ralph" Tenthani bado ni mwakilishi wa BBC nchini Malawi.

Akifanya Interview



Mpenzi Msomaji wetu,Tunapenda kukutumia Habari zetu zote mara tu Tunapoziweka Mtandaoni.Kujiunga nasi Bonyeza Hapa "HABARI" VITUKO "MAPENZI"MAGAZETI,UDAKU>
Endapo una Habari,Picha,Video,Tangazo au Tatizo Lolote wasiliana nasi kwa namba  +255 688 405 951

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post