Kijana
mmoja ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja, usiku wa
kuamkia leo amepigwa risasi ya shingo na watu wasiojulikana wakati
akiingia Club Maisha ilioko Oyster Bay jijini Dar es salaam.
Tukio hilo lilitokea
majira ya saa tano(5) usiku ambapo kijana huyu akiwa na rafiki zake
wanne(4) wakiwa ndio wanashuka kwenye gari yao waliyokuja nayo,
walijikuta wamevamiwa na watu wawili wasiojulikana na yeye kupigwa
risasi ya shingo kisha watu hao kutokomea kusikojulikana.
Shuhuda wa tukio hilo
alisema aliwaona watu wawili walioshuka kwenye gari ndogo nyeusi
ilifunga breki kwa kasi kwani walionekana walikuwa mwendo kasi sana,
kisha kuwavamia watu waliokuwa wanashuka kwenye gari ilikuwa imepaki
muda mfupi baada ya kufika eneo hilo.
shuhuda huyo aliendelea kwa kusema
alisikia sauti ndogo ya kitu kilicholia "pyuuu!!!" bila ya kuelewa ni
nini na kisha kufuatiwa na kelele nyingi za watu hao waliokuwa
wamevamiwa.
Waliotenda tukio hilo walitoweka mara moja eneo la tukio
baada ya watu kujaa eneo ambalo kijana huyo alipigwa risasi alikuwa
ameanguka chini.
Polisi walifika eneo la
tukio na kukuta kijana huyo ameanguka chini na damu nyingi zikiwa
zimemtoka sehemu za shingoni na kifuani huku akiwa amewekewa nguo
shingoni ili damu isiendelee kutoka ambapo ilisemekana ilikuwa ikitoka
nyingi sana.
Walimpakia kwenye gari yao kumuwahisha katika hospitali ya
jirani ya mwananyamala, lakini kijana huyo alifia njiani akikimbizwa
kuelekea hospitali.
Social Plugin