Moja ya vitu ambavyo vimekuwa muhimu
kwenye chakula cha mwanadamu ni chumvi ambayo hutumika kuongeza ladha ya
chakula ambacho hutumika mezani, umuhimu wa kiungo hiki umefikia hatua
ya waswahili kuibatiza chumvi jina la utani ambalo ni Mkuu Wa Jiko,
kiungo hiki kinaweza kuwa na madhara pale ambapo inatumika kuliko
kawaida na madhara hayo ni kwa afya ya mtumiaji .
Je chumvi ni mbaya kwa Afya yako?
Mwili wa mwanadamu unahitaji chumvi kwa
kiwango fulani kwani inasaidia kuongeza madini ambayo mwili wako
unayahitaji hatari ni pale unapokula chumvi nyingi kuliko kiwango
ambacho mwili wako unahitaji.
Imegundulika kuwa chumvi husababisha
matatizo ya shinikizo la damu hali ambayo inaweza ikaongeza uwezekano wa
mtu kupata matatizo ya shambulio la moyo pamoja na hatari nyingine za
magonjwa ya moyo, inashauriwa utumiaji wa chumvi kwa kiwango cha chini
ili kuepukana na matatizo haya.
Je kiasi gani cha chumvi kinazidi kiwango cha kawaida?
Hupaswi kula zaidi ya gramu tano za
chumvi kwa siku, hii ni sawa na kijiko kimoja cha chai ambacho kina
ujazo wa miligram 5, inajumuisha chumvi ambayo unaongeza ukiwa unapika
jikoni, chumvi unayoongeza mezani wakati wa kula na ile chumvi ambayo
inapatikana kwenye chakula kiasili hii ni kwa sababu kuna vyakula
ambavyo ndani yake kuna chumvi hata kama havina ladha ya chumvi kama
vile mikate, Sausage na nyama za kusaga, supu ya kutengenezwa kiwandani,
vyakula vya nafaka ambavyo hutumika kwenye kifungua kinywa (breakfast)
na hata baadhi ya biskuti.
Je tunatumia chumvi nyingi kuliko kawaida?
Waafrika wengi huwa na kasumba ya
utumiaji wa chumvi kwa kiwango kikubwa kuliko kawaida na hii imezoeleka
sana kuanzia majumbani mpaka mahotelini.
Ni rahisi sana kutumia chumvi nyingi kuliko kawaida wakati wa milo ya kila siku.
Nusu ya chumvi ambayo hutumiwa na watu
ni chumvi inayopatikana kwenye vyakula hasa vile vya kutengenezwa
viwandani ambayo huwekwa wakati wa utengenezaji wa vyakula hivi huko
huko viwandani ili kuvifanya vikae kwa muda mrefu, nusu nyingine ni ile
ambayo ambayo huongezwa jikoni na ile ambayo watu huongeza mezani wakati
wa kula ili kukoleza ladha ya chakula husika.
Nini kinatengeneza chumvi?
Chumvi inatengenezwa na vitu viwili
ambavyo ni sodium na chloride, sodium ni sehemu ya chumvi ambayo ambayo
huongeza presha ya damu au kwa lugha inayoeleweka zaidi huongeza
shinikizo au msukumo wa damu hasa pale unapotumia chumvi nyingi kuliko
kiwango cha kawaida, taarifa zinaoandikwa kwenye vihifadhi vya vyakula
hasa vile ambavyo vinatengenezwa viwandani huonyesha kiwango cha madini
ya sodium ambayo yametumika kwenye chumvi, kijiko kimoja cha chai mara
nyingi huwa kina miligramu 2000 za sodium.
Ni jinsi gani tunaweza kutumia kiwango cha chini cha chumvi kwenye vyakula ?
Haiwezekani kupunguza kiwango cha chumvi ndani ya siku moja au ghafla
, mabadiliko yanapaswa kufanyika hatua moja baada ya nyingine .
Muhimu ni kujizoesha hisia ya kudhani kuwa chakula kina ladha hata pale ambapo chumvi haijakolea
Kama una kawaida ya kuongeza chumvi nyingi mezani hatua ya kwanza ni
kuondoa kile kikopo kidogo cha chumvi mezani hasa wakati wa chakula ,
hii ni kwa sababu unapaswa kukumbuka kuwa kama ulishaongeza chumvi tangu
jikoni hauna sababu ya kuongeza nyingine mezani .
Jaribu pia kupunguza kiwango cha chumvi
unachoongeza wakati wa mapishi yako, unapaswa kuonja wakati ukiwa
unapika ili kuepuka kuongeza kiwango cha chumvi ambcho kinaweza kuwa
hatari kwa Afya yako, kama chakula chako kina viungo ambavyo ndani yake
kuna chumvi ya asili hupaswi kuongeza chumvi nyingine juu yake.
Katika tafiti zilizofanyika hivi
karibuni imefahamika kuwa kuna baadhi ya vitu vinavyoweza kutumika kama
chuimvi ambavyo havna madhara sawa na ya chumvi kwenye mwili wa
mwanadamu na mojawapo ni limao pamoja na ndimu.
Kiungo kingine kinachoweza kuchukua nafasi ya chumvi kwenye chakula chako ni mdalasini .
Unataka kujua vyakula visivyo na chumvi nyingi?
Vyakula ambavyo havijatengenezwa
kiwandani kwa maana ya vyakula halisi mara nyingi huwa havina chumvi
nyingi na hii inamaanisha kuwa unapaswa kuchagua vyakula vya asili
kuliko vile ambavyo vimetengenezwa viwandani.
Endapo una Habari,Picha,Video,Tangazo au Tatizo Lolote wasiliana nasi kwa namba +255 688 405 951
Social Plugin