VIRUSI WA CHADEMA WATIMULIWA HUKO KOROGWE


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Jimbo la Korogwe Mjini, kimeanza kuwashughulikia  waliokuwa wanachama wake  baada ya kudai kuwa ni virusi kwa kukikosesha ushindi katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika Desemba 14, mwaka huu.
Miongoni mwa waliotimuliwa ni pamoja na waliokuwa wagombea katika uchaguzi wa serikali za mitaa kwa mwaka huu nchini na kusababisha Chadema kupata kura sifuri katika jimbo hilo.

 
Kwa mujibu wa Katibu wa jimbo hilo, Ezekiel  Mbwilo   hatua hiyo ni moja ya chama hicho kujisafisha kwa kuwatimua wanachama wake 42 miongoni mwao wakiwamo waliokuwa wakiwania uongozi  kwenye uchaguzi huo kwa tuhuma za kukihujumu chama.
Mbwilo alisema Kwamsisi wametimua wanachama sita, Mahenge (10), Kitifu (25) na Manundu kati ni aliyekuwa mgombea wa uenyekiti  anayedaiwa kurubuniwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) hivyo kujitoa dakika za mwisho.

Alisema kutimuliwa kwa wanachama hao muda mfupi baada ya kumalizika kwa uchaguzi huo kumetokana na kugundulika kwa baadhi yao  kukihujumu chama kwa kupewa hongo na wapinzani wao.

Akizungumzia kuhusu uchaguzi huo,  Mbwilo alisema uligubikwa na mizengwe na uwazi kutokuwepo huku misingi ya haki ikikosa kuzingatiwa. 
Na Dege Masoli  -NIPASHE

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post