Vijana watatu mkoani Songea wametakiwa kwenda
na wazazi wao kutubu dhambi za kutaka kuiba sanamu la Bikira Maria
katika Kanisa Katoliki la Kigango cha Samora.
Katekista wa Kigango hicho Keneth Mhagama alisema vijana hao walifanya jaribio hilo usiku wa manane baada ya
ibada ya mkesha ambapo walinzi walifanikiwa kuwadhibiti kabla
hawajafanikiwa na wakawekwa mbaroni.
Vijana hao ni Ahmed, Mohammed na Leonard ambapo Padri wa Kanisa hilo Cristom Kapinga amesema vijana hao wanatakiwa kutubu la sivyo watawaacha kwenye mikono ya sheria washughulikiwe.
Chanzo cha Habari: Gazeti Mtanzania, December 26.
Social Plugin