Kiongozi mmoja wa dini ambaye alipata umaarufu nchini Kenya kwa
kutabiri mwisho wa dunia mwaka 2006 amezikwa katika kijiji cha Bomet.
Kiongozi
huyo wa madhehebu ya House of Yahweh Willy Kiplangat Sang alizikwa
masaa machache baada ya kifo chake katika shamba la babaake kijijini
Matarmat katika sherehe iliohudhuriwa na jamii yake ,majirani na wafuasi
wa kanisa hilo.
Ndugu za nabii huyo aliyezingirwa na utata
wanasema aliugua ugonjwa wa kifua kikuu nyumbani mwake huko Mauche
kaunti ya Nakuru ambapo alikuwa mkulima na muhubiri.
via>>BBC
Social Plugin