ALIYEKUNYWA POMBE ZA KIENYEJI KUPITA KIASI AFARIKI KWENYE DIMBWI LA MAJI HUKO SIMIYU

 

Mwanamme mmoja aliyejulikana kwa jina la Makoye Malungu(65) mkazi wa kijiji cha Mwakadimu wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu amefariki dunia baada ya kutumbukia katika dimbwi la maji baada ya kuteleza wakati akitokea kwenye klabu ya pombe za kienyeji.

Kamanda wa polisi mkoa wa Simiyu Charles Mkumbo amesema tukio hilo limetokea juzi baada ya Malungu kunywa pombe za kienyeji nyingi kupindukia na akiwa njiani,aliteleza na kutumbukia katika dimbwi hilo na kufariki dunia.

Na Anceth Nyahore-Simiyu

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post