Waandishi wa habari wakifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini |
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga alisema katika
kipindi cha mwezi Januari hadi Desemba 2014 mauaji ya albino yamepungua kwa
asilimia 96 na kwamba hali ya ulinzi na usalama mkoani
Shinyanga inaridhisha kwa kuwa matukio makubwa ya uhalifu yamepungua sana
ukilinganisha na miaka ya nyuma hasa kuishia mwaka 2010.
Mkuu huyo wa mkoa alisema mtandao wa barabara katika mkoa wa Shinyanga una jumla ya kilomita 4862.5
Mkutano huo wa mkuu wa mkoa wa Shinyanga na waandishi wa habari pia ilihudhuriwa na viongozi wa mkoa wa Shinyanga/wakuu wa vitengo mbalimbali,wa kwanza kulia ni mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt Ntuli Kapologwe
Waandishi wa habari wakifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini
Viongozi wa mkoa wa Shinyanga wakifuatilia kilichokuwa kinajiri |
Katika mkutano huo Rufunga alisisitiza umuhimu wa wazazi na walezi kupeleka watoto wao shule kwa wakati kinyume na hapo serikali itawachukulia sheria
Katika taarifa yake Rufunga alisema katika mwaka 2014 jumla ya shilingi 8,645,146,895.10 zilitumika katika kuboresha sekta ya maji kwa kipindi cha Januari hadi Desemba
Katika hatua nyingine alisema tofauti na miaka mingine mwaka jana mkoa wa Shinyanga ulijitosheleza kwa chakula na kuwa na ziada ya tani 466,979.1 za nafaka,mahitaji ya chakula katika mwaka 2014 yalikuwa tani 380,185.4 na mavuno yalikuwa tani 847,164.5
Aidha alisisitiza umuhimu wa wananchi kuendelea kulima zao la mtama hasa katika wilaya ya Kishapu na wilaya ya Shinyanga huku akiwataka wananchi kutunza chakula walichonacho ili kuepuka janga la njaa |
Mkuu huyo wa mkoa pia aliyataja baadhi ya maeneo yanayolalamikiwa sana kwa rushwa katika mkoa wa Shinyanga kuwa ni Jeshi la polisi,mahakama ya Mwanzo nguzo nane,Kizumbi na Maganzo na kwa upande wa ngazi za halmashauri ni upande wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa chini ya kiwango.
Social Plugin