Hapa ni katika makaburi ya Masekelo katika manispaa ya Shinyanga,aliyemo
kaburini ni ndugu wa marehemu(hatukufahamu jina lake mara moja) akimpasua kwa
wembe marehemu Benadetha Steven(35) aliyefariki dunia juzi akitibiwa uvimbe wa
tumboni katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga.
Jamaa huyo aliingia kaburini kisha kufungua jeneza,akaanza kuuchana kwa
wembe mwili wa marehemu,akachinja kuku,kisha kumwagia damu marehemu na
kumwingiza kuku huyo kwenye tumbo la marehemu,akafunika jeneza na ndugu
wakaendelea na mazishi na wananchi kususia mazishi hayo.
Akiwa ndani ya JENEZA kaburini-
Upasuaji unaendelea ,hicho cheusi kwenye jeneza ni tumbo la marehemu ambapo inaelezwa kuwa kwa mujibu wa mila za Wakurya
ukifanyiwa kitendo hicho basi mkosi unaondoka kwenye ukoo na hakuna mtu
mwingine anayeweza kuugua.
Jamaa akipokea kuku wake kisha kumchinja kaburini
Ndugu wa marehemu walisikika wakisema "HATUNA UBAYA WOWOTE,ASANTE MUNGU"
Ndugu wa marehemu akifunika jeneza baada ya kumaliza kazi yake,
Akiwa ndani ya Jeneza la Marehemu akifanya mambo ya kimila,kitendo ambacho
kiliwakera wananchi na kuamua kususia mazishi hayo.
Ndugu wa marehemu akitoka kaburini baada ya kumaliza kazi
Hivi ndivyo kaburi lilivyoachwa na wananchi baada ya kuzira kuzika mwili wa marehemu hali ambayo iliwafanya ndugu wachukue jukumu la kumzika ndugu yao kabla jeshi la polisi kuwakamata
Social Plugin