ANGALIA PICHA-MBUNGE WA MBEYA MJINI JOSEPH MBILINYI ALIVYOPATA AJALI ENEO LA MLIMA KITONGA

Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini,Mh. Joseph Mbilinyi akifanya mawasiliano kwa ndugu na jamaa mara baada ya kupata ajali mbaya na kunusurika kifo,ajali hiyo imetokea eneo la Mlima Kitonga Mkoani Iringa jana.


 Mbunge wa Mbeya mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi  almaarufu 'Sugu', amenusurika kufa katika ajali iliyotokea eneo la mlima Kitonga mkoani  Iringa wakati akitokea jimboni kwake kurudi Dar es Salaam.
Ofisa Habari wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tumain Makene,  jana jioni   aslisema kuwa, Mbilinyi alipata ajali hiyo Kitonga baada ya kumaliza ziara  mjini Mbeya kuwashukuru wananchi baada ya ushindi uliopatikana kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa uliomalizika mwaka jana.

Alisema baada ya kufika eneo hilo walipata ajali na kusababisha gari aina ya Land Cruiser alikuwa amepanda kupinduka  na kusababisha kupata majereha.

Kitonga ni mlima unaotisha wenye bonde upande wa kulia na kushoto na endapo gari linaserereka linatumbukia korongoni.

Makene alisema ndani ya gari hilo walikuwamo abiria wengine  ambao kadhalika wamepata majeraha  na kwamba  hali zao zinaendelea vizuri.

Mr. Sugu akiwa Hospitali.




Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini,Mh. Joseph Mbilinyi (watatu kushoto) akizungumza namna hali ilivyokuwa mpaka kupata ajali hiyo.



Gari hiyo inavyoonekana.


IMG-20150110-WA0039
IMG-20150110-WA0040 (1)
IMG-20150110-WA0040
IMG-20150110-WA0041
IMG-20150110-WA0021
IMG-20150110-WA0023

IMG-20150110-WA0027

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post