Askari
wa jeshi la polisi Tanzania, Sajenti Patrick Kondwa amejiua kwa kujipiga risasi
akiwa katika ofisi yake kwenye ghala lakuhifadhia silaha katika kituo
cha polisi cha wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya(PICHANI)
amekiri kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa chanzo cha kifo hicho bado
hakijafahamika na kwamba jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wa
tukio hilo.
Sajenti Patrick mwenye umri wamiaka 54 ,akiwa katika ofisi yake
kwenye chumba cha kuhifadhia silaha katika kituo cha polisi cha wilaya
ya Mbozi amejipiga risasi mdomoni ambayo imetokea kisogoni na kuondoka
na uhai wake, tukio ambalo limetokea majira ya saa tisa usiku na
kuthibitishwa na kaimu mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya
wilaya hiyo, ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya ileje, Rosemary Staki
Senyamule.
Baadhi ya waombolezaji wamesema kuwa
wamepokea msiba huo kwa masikitiko makubwa hasa kwa kuzingatia kuwa
Sajenti Patrick alikuwani askari mwadilifu na anayeipenda kazi yake.