BABA AAMUA KUMNG'ATA USONI MTOTO WAKE KISA KWANINI ANALIA SANA

police_photo 
 Felipe Deaquino.

Matukio ya unyanyasaji kwa watoto wadogo yameendelea kujitokeza kila kukicha, mwanaume mmoja Felipe Deaquino anashikiliwa na Polisi Stamford, Uingereza kwa kosa la kumg’ata usoni mtoto wake mchanga aliyekuwa akilia.

Polisi walifika nyumbani kwa kijana huyo baada ya kupata taarifa za mtoto huyo kunyanyaswa na kumkuta mke wake ambaye aliwaambia Polisi kwamba ana mgogoro na mume wake baada ya kukuta mate usoni kwa mtoto huyo ambaye ana umri wa miezi sita  mchanga mwenye umri wa miezi 6.

Mwanamke huyo na mtoto wake walipelekwa Hospitali baada ya kugundua mtoto huyo alikuwa na majeraha makubwa usoni upande wa kushoto na alikuwa na alama ya kuchomwa moto kwenye kiganja cha mkono ambapo inasemekana kuwa ilisababishwa na sigara.


Deaquino ambaye umri wake ni miaka 18, alikamatwa na Polisi na kuhojiwa akakiri kumng’ata mtoto wake mchanga huku akisema alifanya hivyo kutokana na mtoto huyo kulia, ameshtakiwa kwa makosa mawili ya kushambulia na baadaye akaachiliwa kwa dhamana ya dola 35,000.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post