BABA AMTOBOA MACHO MWANAYE KISHA KUJINYONGA BAADA YA KUVURUGANA NA MKE WAKE HUKO KAGERA


Mtoto aliyefanyiwa ukatili na baba yake 


Mkazi mmoja aishiye katika Kitongoji cha Buyumba,Kijiji cha Bushemba,Kata ya Buganguzi Wilayani Muleba Mkoa wa Kagera aitwaye Godfrey Joseph Kajuna (45miaka) amejinyonga hadi kufa baada ya kumfanyia ukatili mtoto  wake wa kumzaa.

Inasemekana kuwa baba huyo alimpiga na kumjeruhi kichwani kwa fimbo nzito kisha akamtoboa macho, mtoto huyo aitwaye Agripina Godfrey (12) anayesoma darasa la Kwanza katika shule ya msingi Ilambika.
Chanzo cha habari hizi kinasema kisa kizima ni kwamba Baba alitoka ndani na kuwaambia wanae kuwa Mama yao akirudi wasimfungulie mlango…

Hivyo mama aliporudi watoto kwa kumuogopa Baba yao wakakataa kata kata kumfungulia Mlango.
Basi Mama akaondoka kujiweka sehemu.

Baba yao aliporudi akawauliza Mama yao yuko wapi,ndipo huyo mtoto aliyeonekana kama ndiyo mkubwa kwenye familia hiyo akamjibu Baba yake kuwa "Baba si ulisema mama akija tusimfungulie?" Hali hiyo ikamfanya Baba yake aanze kumpiga sana! Mpaka kumuumiza vile.

Sasa damu zikaanza kumtoka mtoto,Baba mtoto akachukua Chumvi na kuanza kuimimina kwenye jeraha kichwani

Basi mtoto alipoonekana kama hali inakuwa Mbaya… Baba akaandika kijibarua haraka na kusema kuwa kwa kitendo alichofanya na vitendo vingine ambavyo huwa anaifanyia familia hiyo ameogopa kukamatwa… akajitundika kwenye Kamba na kujimaliza yeye mwenyewe. Mtoto alipelekwa katika Hospitali teule ya Wilaya ya Muleba (Rubya Hospital) kwa matibabu zaidi.

Stori Na  Sweetbert Rwabukambara

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post