Balaa la Mwaka mpya 2015 !! WATU 36 WAFARIKI DUNIA PAPO HAPO WAKISHEREHEKEA MWAKA MPYA UWANJANI, KISA NI FEDHA ZA BANDIA!!!!
Thursday, January 01, 2015
Gari la kuchukua wagonjwa baada ya kutokea mkanyagano
Eneo lililotokea vifo vilivyotokana na mkanyagano mjini Shanghai, nchini China
Watu 36 wamepoteza maisha na wengine kiasi ya 40 kujeruhiwa kotokana na
mkanyagano katika hekaheka za kusherehekea mwaka mpya nchini China ambapo fedha bandia zilirushwa kama theluji
Tukio hilo lilitokea wakati umati mkubwa wa watu ukiwa umekusanyika
katika uwanja wa Chen Yi Square.
Shirika la habari la China Xihnua
limemnukuu aliyeshuhudia mkasa huo akisema watu walikuwa wakitaka
kujipatia kuponi ambazo zilionekana kama fedha aina ya dola ambazo
zilikuwa zikirushwa kutoka katika dirisha kutoka gorofa ya tatu ya jengo
moja.
Hatari ilianza kabla ya kuwadia 2015 Serikali ya China ilisema umma huo wa watu ulianza kukanyagana
mapema kabla ya kutimia usiku wa manane, katika mji huo wenye
mchanganyiko wa watu.
Tukio hilo linaelezwa kuwa baya zaidi kutokea
tangu mwaka 2010, baada ya kuzuka moto katika jengo lenye makazi ya watu
na kusababisha vifo vya watu 58.
Chanzo cha mkanyagano huo bado hakijafahamika lakini chombo cha habari
cha serikali na baadhi ya walioshuhudia wanasema kwa sehemu fulani
kadhia hiyo imesababishwa na watu wakiwania kujipatia fedha
zilizoonekana kama ni sarafu halisi. Bwana mmoja kati ya watu 47 waliofikishwa hospitali kwa ajili
ya matibabu alisema fedha bandia zilikuwa zinarushwa kutoka katika jengo
moja ikiwa sehemu za sherehe za mkesha wa mwaka mpya.
Watu walikuwa
wakikimbia kwenda kuchukua kuponi. Alisema mtu huyo ambae
alijitambulisha kwa jina la ukoo la Wu.
Bwana mwingine Cui Tingting, mwenye umri wa miaka 27 alisema alifanikiwa
kupata kiasi fulani cha kuponi hizo lakini alizitupa baadae baada ya
kugunduka kuwa zilikuwa fedha bandia.
"Ulikuwa ukatili sana. Watu
waliokuwa mbele yetu walikuwa tayari wamelala katika sakafu, na baadhi
ya watu walikuwa wakiwakanyaga,"alisema majeruhi huyo.
Televisheni ya serikali ilinukuu wazungumzaji wengine wakisema fedha hizo bandia zilikuwa zikitiririka chini mithili ya theluji.
Kauli ya polisi kuhusu mkasa
Jeshi la polisi mjini Shanghai lilisema halikuweza kuthibitisha kama
fedha hizo bandia ndizo zilizosababisha mkanyagano, na kuongeza kwamba
uchunguzi unaendelea huku likiwataka wananchi waendelee kuwa watulivu
kwa wakati huu.
Milango ya vioo ya jengo ambalo limetajwa kutoa fedha hizo bandia
imeonekana kufungwa Alhamis hii, ingawa ishara za mabaki yalionesha
kulikuwa na shamrashamra kwa wakati uliopita zinaonekana katika sakafu
yake.
Kwa kupitia televisheni ya taifa ya nchi hiyo Rais Xi Jinping ameitaka
serikali ya Shanghai kutafuta chanzo cha tukio hilo haraka iwezekananvyo
na kuamuru serikali katika maeneo yote nchini China kuhakikisha kwamba
mkasa kama huo hautokei tena.
Social Plugin