Kumekuwa na story jioni ya leo Dar
kuhusu kikundi cha watu cha ‘Panya Road’ kuvamia maeneo mbalimbali,
kupora vitu na kupiga watu.
Kamanda wa Polisi Suleiman Kova amezungumza kupitia kituo cha TBC1,
amesema kuwa wananchi wanapaswa kuwa na amani kwa kuwa kikundi hicho
kina wahalifu wachache, tayari kuwa wawili ambao wamekamatwa na
oparesheni inaendelea ili kuwadhibiti.
“Sisi
kama Jeshi la Polisi tumepata taarifa vilevile kama walivyopata watu
wengine, kwamba hao vijana maarufu kwa jina la ‘Panya Road’ walikuwa
wamezagaa maeneo mengi…”– Kamanda Kova.
“Hawa
ni vijana ambao hawana kazi… hawana maadili mazuri… kwanza tuzungumzie
uzito wa tatizo, jinsi ambavyo habari zilivyovuma zimevumishwa kubwa
zaidi kuliko uzito wa tukio lenyewe… Nataka niwaambie wananchi kwamba
endeleeni na shughuli zenu…”
Hatukatai kwamba hawa vijana wapo.. lakini nasema suala limekuzwa limetiwa hofu, watu wamepata hofu kupindukia …”
Wale wanaopeleka uvumi waache kwa sababu wewe hujaona tukio, ukiletewa message na wewe unampelekea mtu mwingine hiyo sio sahihi…”
Tutashughulikia
suala la ‘Panya road’ na leo doria inaendelea usiku kucha, wananchi
waondoe hofu wajue jeshi la Polisi lipo… Haiwezekani panya road
wakatawala Dar es Salaam… Haiwezekani panya road wawe na nguvu kuliko
jeshi la Polisi…”
Wamekamatwa wawili… tuliwakamata muda mfupi tu baada ya kuanza vurugu zao…”– Kamanda Kova.
Social Plugin