Pichani ni Daktari
wa Zahanati ya Nyankumbu iliyopo mkoani Geita Josephat Msafiri akipata kichapo baada ya kukutwa akilewa muda wa kazi-picha kutoka maktaba ya malunde1 blog |
Mwandishi wa
Gazeti la Mwananchi Mkoa wa Geita Jackline Masinde,ametishiwa kuuawa na Daktari
wa Zahanati ya Nyankumbu iliyopo mkoani Geita Josephat Msafiri.
Inaelezwa
kuwa tarehe 23 Desemba mwaka jana
Mwandishi huyo aliripoti taarifa za Daktari huyo kuwafungia nje wagonjwa kisha
kwenda kulewa pombe na kuacha wagonjwa
wakiwa wamezidiwa katika kituo alichokuwa akifanyia kazi cha Nyakabale hapo awali .
Hali hiyo
ilisababisha wagonjwa kumfuata baa alikokuwa akilewa pombe kisha
kumwadhibu kwa viboko ,ambapo taarifa hiyo ilisababisha daktari kuvuliwa madaraka yake kisha kuhamishwa kituo
chake cha kazi na kupelekwa kituo cha Nyankumbu na mwajiri wake ambaye ni mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa
Geita Magreth Nakainga.
Mwandishi
huyo alisema juzi majira ya saa 5:23 asubuhi alimpigia Daktari huyo ikiwa
nimoja wa wajibu wake wa kazi akihitaji taarifa za kitaalam kuhusu madhara ya
sumu ya Zebaki ofisini kwake .
“Nilimpigia
simu daktari nikihitaji taarifa za madhara ya sumu ya Zebaki ,alipokea simu
na kuanza kunitolea lugha za matusi (tunazihifadhi kwa sababu ya maadili) huku
akinitishia kuniua kwa kusema "nikionana nawewe sehemu yoyote haki ya mungu
nakuua”,alimnukuu Daktari huyo.
Alisema
alipomuhoji kwanini anamtishia kumuua,daktari huyo alisema ana uchungu na taarifa
alizozitangaza nchi nzima kuhusu yeye kupigwa na wagonjwa ,kuwa imemuathiri katika maisha yake.
Mwandishi
huyo alisema kuwa kauli hiyo ya Daktari ilimpa mashaka kisha kutoa taarifa kituo cha
Polisi cha Wilaya ya Geita mkoani humo na kufungua kesi namba GE/RB/366/2015 ya
kutishiwa kuuawa kwa njia ya mtandao.
"Niliamua
kutoa taarifa polisi na mtuhumiwa mpaka sasa amekamatwa ,alipohojiwa alikiri
kufanya kosa na kuomba msamaha mbele ya polisi"alisema Masinde.
Mwandishi huyo wa habari sasa yuko katika wakati mgumu kutokana na kufichua maovu mengi katika jamii na amekuwa akipata vitisho mbalimbali kutoka kwa
baadhi ya viongozi ambao wamekuwa wakimtishia kumpeleka mahakamani kwa
kile kinachoelezwa kuwa anawaandika vibaya,huku pia akinusurika kupigwa
na kuharibiwa vifaa vyake vya kazi.
Na Valence Robert-Malunde1 blog Geita
Endapo una Habari,Picha,Video,Tangazo au Tatizo Lolote wasiliana nasi kwa namba +255 688 405 951