DEREVA WA PIKIPIKI NA ABIRIA WAKE WAFARIKI KWA KUGONGWA NA LORI MJINI KAHAMA

Mwendesha pikipiki aitwaye Jackson Alfred(22) mkazi wa Ngalama-Kakonko mkoani Kigoma na abiria wake Kashindye James(6) ambaye ni  mtoto wa kike wamefariki dunia mjini Kahama, baada ya pikipiki waliyokuwa wamepanda kugongwa na lori.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha, tukio hilo limetokea jana mchana katika kijiji cha Igomelo kata Malunga, wilayani Kahama.

Amesema gari lenye namba T679 AUN aina ya Mitsubishi Fuso Tiper mali ya Issa Obeid Mkwale mkazi wa Ngara ikiendeshwa na Athuman Juma(35) mkazi wa Nyakato-Kahama iligonga pikipiki hiyo yenye namba za usajili MC.993ACX aina ya Sunlg.

Kamanda Kamugisha amesema Jackson Alfred alifariki dunia papo hapo, huku mtoto Kashindye James ambaye alikuwa abiria akifariki dunia jana saa 12 jioni wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya ya Kahama.

Hata hivyo Kamanda Kamugisha amesema jeshi la polisi linafanya uchunguzi wa chanzo cha ajali hiyo na kuongeza kuwa dereva wa gari hilo anashikiliwa na polisi kwa hatua zaidi za kisheria.
Na Kadama Malunde-Shinyanga 


Bonyeza hapa Tukupe habari zote mara moja zikitoka  
Endapo una Habari,Picha,Video,Tangazo au Tatizo Lolote wasiliana nasi kwa namba  +255 688 405 951

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post