GAZETI LENYE KIBONZO CHA MTUME "FRONT PAGE" LAUZWA KAMA NJUGU

 
Gazeti la Charlie Hebdo leo limeanza kusambaza toleo la gazeti lake ambalo limechapishwa kibonzo cha Mtume Mohammad kwenye ukurasa wake wa mbele.


Nakala Milioni za gazeti hilo zimeanza kusambazwa na nyingine zitafuata iwapo wanunuzi wataongezeka.
Picha ya kibonzo hicho iliyopo ukurasa mbele wa gazeti hilo inamwonyesha Mtume Mohammad akilia.

Wandishi wa jarida la Charlie Hebdo wamechapisha tena picha ya kibonzo cha mtume Muhammad 
 
Wachambuzi wa mambo wanaona kuwa picha hiyo itachochea chuki.

Hata hivyo waandishi wa habari wa gazeti hilo wanasema ukurasa wa mbele unamaanisha Waandishi wa habari wamewasamehe waliotekeleza shambulizi la kigaidi lililofanyika Jumatano wiki iliyopita.

Naibu Mhariri wa Gazeti la Liberalation Alexandra Schwatzbrod anasema ulikuwa uamuzi mwepesi kwa gazeti lake kuchapisha picha ya kibonzo hicho.

Chanzo-BBC Swahili

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post