Hatari Aisee!! JAMAA AGOMBANA NA MKE WAKE,AMUUA KWA KUMPIGA RISASI MBELE YA POLISI

Mara nyingi kituo cha Polisi ni mahali ambapo mtu anakuwa na uhakika wa kuwa na usalama, kuna matukio yakitokea katika maeneo hayo huwa ni ya kushtua, mojawapo ni kama hili la mwanaume mmoja kumuua mke wake na kisha kujiua mwenyewe wakiwa katika kituo cha Polisi cha Parkview, Johannesburg Afrika Kusini.


Mtu na mkewe walifika katika kituo cha Polisi kwa ajili ya kupeleka malalamiko ya mgogoro wa kifamilia waliokuwa nao, wakiwa wanatoa maelewano kila mmoja, mwanaume aliomba akachukue miwani yake ya kusomea katika gari, aliporudi alikuja akiwa na bastola, akampiga mke wake na kumuua, kisha akawanyooshea askari waliokuwa zamu, mwisho akajiua mwenyewe. 

Watu hao walifikishwa katika kituo cha Polisi wakiwa katika magari tofauti, walikuwa na ugomvi katika nyumba yao Johannesburg ambapo Polisi walifika na kuamua kuwachukua kwenda nao kituoni hapo ili wakatafute suluhu ya ugomvi huo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post