JUMLA ya watoto 76 wamezaliwa katika mkesha wa Mwaka Mpya katika jiji
la Dar es Salaam, huku akinamama wakishauriwa kutobeba mimba katika
kipindi cha baridi ili kujifungua wakati wa msongamano mdogo hospitali.
Watoto hao wamezaliwa katika Hospitali za Amana, Mwananyamala, Temeke
na ya Taifa Muhimbili, huku kati yao 14 wakizaliwa kwa njia ya
upasuaji.
Katika Hospitali ya Amana, Ofisa Muuguzi wa Zamu, Rose Mkondola
alisema watoto waliozaliwa katika hospitali hiyo ni 25 huku waliozaliwa
kwa upasuaji ni watano, ambapo watoto na wazazi hali zao zinaendelea
vizuri.
Alisema kipindi hiki, idadi wa akinamama wanaojifungua ni wachache,
kutokana na wanawake wengi hubeba mimba katika kipindi cha baridi na
hivyo kujifungua katika kipindi cha kuanzia mwezi Machi.
“Hali zao zinaendelea vizuri na baadhi yao wameruhusiwa, kipindi hiki
akinamama wamekuwa wachache kwa sababu ni kama huwa wana msimu, huwa
tunawashauri wasibebe mimba katika kipindi cha baridi kwa sababu
msongamano unakuwa mkubwa na wahudumu wachache kwa hiyo ni vurugu,”
alisema.
Kwa upande wa Hospitali ya Mwananyamala, Muuguzi Kiongozi Rehema
Kessy alisema watoto waliozaliwa hospitalini hapo ni 23, ambapo kati yao
wa kiume ni 18 na wa kike watano.
Alisema hali za watoto na mama zao ni za kuridhisha, kutokana na
huduma nzuri walizopata hospitalini hapo. Katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili, Kaimu Muuguzi wa Wadi ya Wazazi, Renalda Kisheo alisema,
watoto waliozaliwa katika hospitali hiyo ni tisa, wa kiume watatu na wa
kike sita.
Alisema watoto saba kati yao, walizaliwa kwa njia ya upasuaji huku
wawili wakizaliwa kwa njia ya kawaida. Hata hivyo, alisema mtoto mmoja
alifariki baada ya kuzaliwa.
“Wote wako salama wazazi na watoto wao, isipokuwa huyo mtoto mmoja
ambaye alifariki muda mfupi baada ya kuzaliwa, lakini wagonjwa wote
wanaendelea vizuri,” alisema.
Muuguzi wa Hospitali ya Temeke, Rolester Kinunda, alisema katika
hospitali yake wamezaliwa watoto 19, kati yao wakiume 10 na wa kike 9.
Kinunda alisema kati yao, mmoja amezaliwa kwa njia ya upasuaji na wazazi
na watoto wao wanaendelea vizuri.
Bonyeza hapa Tukupe habari zote mara moja zikitoka "HABARI" VITUKO "MAPENZI", MAGAZETI,UDAKU>
Bonyeza hapa Tukupe habari zote mara moja zikitoka "HABARI" VITUKO "MAPENZI", MAGAZETI,UDAKU>
Endapo una Habari,Picha,Video,Tangazo au Tatizo Lolote wasiliana nasi kwa namba +255 688 405 951
Social Plugin