AUAWA KWA KUCHINJWA KAMA KUKU NA RAFIKI WA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII BAADA YA KUONANA LIVE!!




Bedner aliuawa na rafiki yake baada ya kukutana kwa mara ya kwanza
Kijana mmoja mwenye mienendo ya kustaajabisha nchini Uingereza, alipiga simu kwa polisi baada ya kumchinja mwenzake mwenye umri wa miaka 14 ambaye walifahamiana tu kupitia mtandao ya kijamii.

Kijana huyo alipigia polisi simu na kuwaambia kwamba angependa waende nyumbani kwake huku wakiandamana na wataalamu wa uchunguzi wa mauaji kwani alikuwa amemuua rafiki yake.

Kijana huyo kwa jina Lewis Daynes mwenye umri wa miaka 19 , ametajwa na polisi kuwa kijana hatari, mhalifu ambaye anawahadaa wenzake na kisha kuwadhuru.

Inaarifiwa ilikuwa mara ya kwanza kwa wawili hawa kukutana uso kwa uso kwani suiku zote mawasiliano yao yalikuwa kupitia internet.

Daynes, alifungwa jela maisha baada ya kupatikana na hatia ya kumuua Breck Bednar mwaka jana.

Daynes kutoka Grays, Essex, alimwalika Bednar nyumbani kwake baada ya kujuana tu kupitia internet akimwambia alitaka sana kumuona.

 Bedner alipowasili nyumbani kwa Daynes, Daynes alimfunga mikono yake na kisha kumuua.


Daynes ametajwa na polisi kama kijana hatari
Taarifa hii ya kijana huyo kuwapigia polisi simu na kuwaarifu kuhusu mauaji aliyoyafanya, imeibuka  jana siku moja baada ya hukumu kutolewa dhidi yake.

'ninahitaji polisi kuja nyumbani kwangu,'' alisema kijana huyo na alipoulizwa ikiwa alikuwa anakiri kufanya mauaji akaseme, '' Ndio , ninakiri. ''

Baadaye aliwapa polisi taarifa zake, jina lake na alikoishi na kisha kuwashukuru. Alidai kwamba alimuua rafiki yake Breck baada ya kumtisha kwa kisu.

''Sikumbuki kilichotokea lakini nilimchinja, '' aliwaambia polisi.

Baadaye polisi walifika nyumbani kwake na kumpata Daynes akiwa mtulivu huku mwili wa rafiki yake ukiwa sakafuni.


Mamaake Bedner(pichani) amesema vijana wanapaswa kutahadhari wanapojihusisha na maswala ya mitandao
Daynes, ametajwa kama kijana ambaye hakueleweka kitabia ila alipenda sana kutumia muda wake kwenye kompyuta. 

Wazazi wake waliachana hali iliyosababisha maafisa wanaoshughulika maslahi ya watoto kumpeleka kwa familia ambayo sio yake ili aweze kutuzwa.

Alikatakata nguo alizokuwa amezivaa akijaribu kuharibu komputa aliyokuwa anaitumia ili kufuta ushahidi wa mazungumzo waliyokuwa nayo na rafiki yake kabla ya kumuua.

Kabla ya kuwapigia polisi simu, alimtumia mtu mmoja picha ya mwili wa Bednar ushahidi wake kwamba amemuua. 

Hata hivyo polisi wangali wanachungaza kumtambua mtu huyo.

Mamake kijana aliyeuawa amesema anatuami kuwa kisa cha mwanake kitakuwa funzo kwa vijana wanaojihusisha na michezo ya kwenye internet. 
Via>>BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post