Hili Jipya!! MKE AUA MME WAKE KWA NYAMA YA MBUZI

Mkazi wa kijiji cha Nakachindu kata ya Mkundi Halmashauri ya wilaya ya Masasi mkoani Mtwara, Asumini Bakiri (39) amefikishwa mahakamani kujibu shitaka la mauaji linalomkabili la kumuua mumewe, Simoni Simoni (45).

Alifikishwa mahakamani jana na kusomewa shitaka lake na Mwendesha Mashtaka, Iddi Shabani mbele ya Hakimu wa Mahakama ya wilaya ya Masasi, Halfani Ulaya.

Alidai kuwa mshtakiwa huyo, alitenda kosa hilo Januari Mosi mwaka huu huko katika kijiji cha Nakachindu wilayani Masasi saa 1:00. Anadaiwa kumuua kwa kile kinachodaiwa ni sumu baada ya kutokea ugomvi kati yao.

Iddi alidai kuwa siku ya tukio, mume alinunua mapupu yanayoliwa pamoja na nyama ya mbuzi nusu kilo kwa ajili ya sherehe ya Mwaka Mpya, lakini katika hali ya kushangaza usiku ulipofika alihitaji chakula, lakini mkewe alidai kuwa hakuna unga na kwamba angeenda jirani kuomba.

Akiwa ametoka nyumbani kwenda jirani kuomba unga huo, mume alianza kula nyama na baada ya kumaliza alianza kutokwa na povu jeupe kinywani mithili ya mtu aiyepewa sumu huku hizo nyama zikiwa zimekwama shingoni mwake.

Mkewe alipofika alimkuta mumewe akiwa ameshapoteza fahamu na alifariki dunia akiwa kwenye pikipiki, wakati akipelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu. Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa Simoni aliwekewa sumu kwenye nyama hiyo.

Mshitakiwa alirudishwa rumande na kesi iliahirishwa hadi Januari 19 mwaka huu itakapotajwa tena.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post