Huenda huruma yake kwa viumbe hawa ndiyo iliyomponza na kusababisha mauti ya watu waliokuwa katika gari alilokuwa akiendesha.
Mwanamke mmoja Emma Czornobaj raia
wa Canada, amejikuta na hatia kutokana na kufanya uzembe ambao
umesababisha ajali mbaya ya gari, alisimamisha gari ghafla katika
barabara kuu kwa lengo la kuwaacha bata wakiwa kwenye kundi kubwa wavuke
barabara na kusababisa kutokea kwa ajali na vifo vya watu wawili.
Gari lililokuwa linakuja nyuma liligonga kwa nyuma ya gari la mwanamke huyo na kusababisha kifo cha Andre Roy na binti yake Jessie mwenye umri wa miaka 16, Czornobaj alisikitika pale aliposimama na kukusanya bata wote na kuwaweka kwenye gari lake.
Mwanamke huyo alikutwa na makosa mawili,
kuendesha gari kwa kasi na uzembe, amehukumiwa kukaa jela siku 90
pamoja na kuihudumia jamii kwa saa 240, pia amepigwa marufuku kuendesha
gari kwa muda mwa miaka kumi.
Social Plugin