JAMAA AKUTWA AMEFARIKI DUNIA AKIWA UCHI WA MNYAMA

Mwanaume mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 25 amekutwa akiwa amefariki dunia maeneo ya Stanley Road Katika Manispaa ya Kigoma-Ujiji huku akiwa hana nguo.

Akitoa taarifa hiyo kwa waandhishi wa habari hapo jana, Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Kamishina Msaidizi ACP  Japhari Muhamed, alisema kuwa mwili huo uliokotwa jana majira ya saa 1:00 asubuhi baada ya wananchi kuuona na kutoa taarifa Polisi.

Kamanda alisema kuwa chanzo cha kifo hicho hakijafahamika hata jina lake halijafahamika na wala ndugu zake hivyo mwili umehifadhiwa mochwari ili kusubiri kama kuna ndugu atakaye jitokeza.

“Hata hivyo jana marehemu alionekana mtaani akitembea uchi kama mtu mwenye matatizo ya akili, uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea” alisema kamanda.

Wakati huohuo, Gereminye Kigonza mkazi wa kijiji cha Kazilamiunda kata ya Kasanda Zone 22 Wilaya ya Kakonko mkoa wa Kigoma amefariki dunia baada ya kupigwa na radi iliyosababishwa na mvuo kubwa iliyokuwa ikinyesha.

Kamanda alisema kuwa tukio hilo lilitokea mapema wiki hii majira ya saa 10 jioni wakati mvua kubwa ikinyesha.

“Kwa kipindi hiki mkoa huu umekuwa na mvua nyingi ambazo zinaambatana na radi ambazo zimekuwa zikileta madhara” alisema Kamanda.

Hata hivyo Kamanda aliwataka wananchi kutokaa katika maeneo hatarishi wakati wa mvua na kuwa waangalifu kwa matumizi ya vifaa vinavyotumia umeme wakati wa mvua za  radi.

Chanzo...E.Senny

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post