JAMAA ALIYEPIGWA NA ASKARI MAGEREZA SHINYANGA MJINI BAADA YA KUWANYIMA SODA NA BISKUTI ,ABURUZWA MAHAKAMANI



Picha ya majeraha aliyopata mwananchi aliyeshambuliwa na askari Magereza Shinyanga.

Hatimaye mkazi wa kijiji cha Nhelegani manispaa ya Shinyanga Lugenzi Maguta (45), aliyeshambuliwa kwa kipigo na askari magereza wa gereza la wilaya ya Shinyanga baada ya kuwanyima soda na biskuti amefikishwa mahakamani na kusomewa shitaka la kufanya fujo gerezani.

Maguta amefikishwa katika mahakama ya mwanzo Shinyanga mjini ambapo upande wa mashitaka ulimsomea shitaka la kuingia gerezani na kufanya fujo akidaiwa kulazimisha kumpatia soda na biskuti ndugu yake aliyekuwa mahabusu shitaka ambalo mshitakiwa amelikana.
 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post