Kukamatwa kwa jamaa aliyegonga ukuta wa
Kituo cha Polisi akiwa anaendesha gari huenda ilikuwa moja ya kazi
ambazo zilikuwa rahisi zaidi kwa Polisi wa kituo cha Frodsham,
Uingereza.
Polisi wamesema jamaa huyo alikuwa
amelewa, alipata ajali hiyo alipokuwa akitoka na gari yake katika eneo
la Parking ambayo iko jirani na kituo hicho, akapoteza mwelekeo na
kugonga ukuta wa kituo hicho.
Polisi walimkamata na kugundua amelewa, akapandishwa kizimbani kwa kosa la kuendesha gari akiwa amelewa.
Social Plugin