Kimenuka!! CCM YAWATANGAZIA VITA WANAOFANYA KAMPENI ZA URAIS NA WAPAMBE WAO


Chama cha Mapinduzi CCM,kimesema hakitasita kuwachukilia hatua kali za kimaadili wanachama na viongozi wa chama hicho ambao wameendelea na kampeni za kuwania nafasi za juu za chama hicho ikiwemo ile ya uraisi kabla ya wakati,kuwatahadharisha juu ya usambazi wa taarifa zisizosahihi kwa hofu ya kuchukuliwa hatua na kuwataka kujidhibiti na kudhibiti wapambe wao.

Akiongea na vyombo ya habari mjini Zanzibar,katibu wa itikadi uenezi wa CCM ndugu Nape Nnauye amesema chama hakitasita kuchukua hatua kali kwa wanachama na viingozi ambao wameendelea kukaidi agizo la kamati kuu la kuwataka kutojihusha na kampeni kabla ya wakati.
 
Aidha Nape amesema chama kimewataka wanachama na viongozi hao,kuwadhibiti wapambe wao ambao wamekuwa wakitoa taarifa potofu pindi vikao vya kamati kuu inapoketi na kusema kuwa chama hicho kina kazi nyingi za kufanya si kujadili wagombea pekee.

Kuhusu kamati ya maadili iliyoketi tarehe 19 mwezi wa kwanza 2015,Nape amesema kuwa mambo yote yaliyojadiliwa katika kamati hiyo yatawakilishwa kwenye kamati kuu kwa kujadiliwa na ndipo yatatolewa kwa wanannchi na kuwataka wagombea kutokuwa na hofu kama wanahisi wako sahihi kimaadili.
Via>>Itv
Bonyeza hapa Tukupe habari zote mara tu Tunapozitoa "HABARI" VITUKO "MAPENZI"MAGAZETI,UDAKU>
Endapo una Habari,Picha,Video,Tangazo au Tatizo Lolote wasiliana nasi kwa namba  +255 688 405 951

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post