Baada ya kizaa zaa kwenye makaburi ya Masekelo katika manispaa ya Shinyanga juzi kuhusu maiti kupasuliwa tumbo kwa wembe kisha kuku kuzikwa na marehemu,leo jipya jingine limetokea asubuhi mjini Shinyanga,angalia matukio katika picha hapa chini
|
Diwani wa kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga,
Sungura George (mwenye shati la pundamilia)aliyepita jirani na ofisi hizo za CCM akitokea ofisi za afya za
manispaa ya Shinyanga akisukumwa na Vijana wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini baada ya kuvamiwa ghafla na
vijana hao na kushambuliwa kwa kuchapwa makofi matatu.
Vijana wa CCM takribani 20 leo asubuhi walifika kwenye ofisi za CCM wilaya na kufunga ofisi za chama hicho wakishinikiza viongozi wa ngazi ya wilaya waondolewe katika chama kwani wamekuwa wasaliti, matokeo yake chama kimepoteza mitaa,vijiji na vitongoji vingi katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka jana -picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog
|
|
Msamaria mwema akimwondoa diwani wa Chadema Sungura George baada ya kushambuliwa na vijana wa CCM na kusurika kugongwa gari,ambapo bila msamaria mwema huyo,diwani huyo angegongwa na gari.Ofisi za CCM wilaya zipo karibu na barabara -picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog |
|
Vijana wa UVCCM wakiwa eneo la tukio-picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog |
|
Vijana wa UVCCM wakiwa kwenye ofisi za chama chao. |
Viongozi wanaolalamikiwa ni katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini,Charles Sangula,katibu mwenezi wa wilaya, Charles Shigino na mchumi wa
wilaya Ahmed Mapalala ambapo UVCCM wanataka waondolewe kwenye chama wakidai kuwa sio waadilifu na wanawadharau UVCCM-picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog
|
Vijana wa UVCCM wakimsikiliza mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Kanali mstaafu Tajiri Maulid aliyefika katika ofisi
hizo baada ya kupata taarifa, aliwasihi vijana hao wafuate utaratibu kwa
kuandika barua na kuwasilisha malalamiko yao-picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog |
|
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Kanali mstaafu Tajiri Maulid aliyefika katika ofisi
hizo baada ya kupata taarifa, aliwasihi vijana hao wafuate utaratibu kwa
kuandika barua na kuwasilisha malalamiko yao-picha na Marco Maduhu-Malunde1 blog
Ikumbukwe kuwa
Desemba
15,2014 majira ya saa 5 na nusu asubuhi,katibu wa Siasa na uenezi wa CCM wilaya
ya Shinyanga Mjini Charles Shigino na katibu wa umoja wa Vijana wilaya ya
Shinyanga Mjini (UVCCM), Zawadi Husein Nyambo walitukanana matusi ya nguoni
almanusura wachapane makonde wakati Shigino akiingia katika ofisi za Chama,
(mlangoni).
Katibu huyo
wa umoja wa Vijana wilaya ya Shinyanga Mjini (UVCCM), Zawadi Hussein Nyambo
alisema alimzuia katibu mwenezi huyo kuingia katika ofisi za chama hicho kwa
madai kuwa yeye ni msaliti wa chama na amekuwa akitoa siri za chama na kuzipeleka kwa
wapinzani.
Katika
uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika Desemba 14,2014, kati ya mitaa 55
katika wilaya ya Shinyanga Mjini, CCM, walipata ushindi katika mitaa 26 huku
(CHADEMA) wakipata mitaa 29, na katika kata ya Ngokolo yenye mitaa 7, CHADEMA
walipata mitaa 6 huku CCM wakiambulia mtaa mmoja pekee, matokeo ambayo
yamesababisha ugomvi ndani ya (CCM) wakisaka mchawi wao.
|
Bonyeza hapa Tukupe habari zote mara moja zikitoka
"HABARI" VITUKO "MAPENZI", MAGAZETI,UDAKU>
Endapo una Habari,Picha,Video,Tangazo au Tatizo Lolote wasiliana nasi kwa namba +255 688 405 951
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin