KUHUSU MAUAJI YA NG'OMBE 5480 HUKO KATAVI

Chama cha wafugaji nchini (CCWT) kimeitaka serikali kutoa kauli juu ya mauaji ya ng’ombe zaidi ya 5480 yaliyofanywa na askari wa wanyamapori kutoka hifadhi ya taifa ya mbuga ya Katavi kwa kipindi cha miaka miwili kufuatia vitendo hivyo kuendelea kila kukicha ambapo hivi karibuni ng’ombe 52 wamepigwa risasi na askari hao huku kukiwa hakuna hatua zozote zinazochukuliwa.


Kauli hiyo inatolewa na katibu wa chama cha wafugaji Tanzania (CCWT) George Kifuko ambapo amesem,a chama hicho kinalaani mauaji ya ng’ombe ambayo yamekuwa yakifanywa na askariw a wanyamapori kila kukicha kwa kisingizio cha ng’ombe kuingika katika hifadhi.
 
Kwa kipindi cha mwaka 2012 mpaka 2014 katika mkoa wa Katavi pekee jumla ya ngombe 5480 wameuwawa kwa kupigwa risasi na askari wa wanyamapori wa mbuga ya Katavi.
 
Katibu huyo pia akaonya baadhi ya wanasiasa ambao wamekuwa wakiwatumia viongozi waliosimamishwa katika chama hicho kujenga migogoro kwa maslahi yao binafsi kwa kuwagawa wafugaji kikabila na kikanda hali ambayo inaweza kuzua migogoro mkubwa katika jamii hiyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post