SABABU ZA WATU KUPENDA KUCHORA TATOO MACHONI

 
Kufungwa jela kwa mhalifu mwenye tatoo kwenye jicho lake mjini Alaska kumezua gumzo sana nchini Marekani kuhusu hatua wanazochukua waru kurembesha nyuso zao.


Bila shaka hili pia limezua gumzo kwani ni kasumba ambayo ndio imeanza kuchipuka na kuwavutia watu wengi sana.

Jason Barnum, mwenye umri wa miaka 39, ambaye alikiri kosa la kujaribu kumuua afisa wa polisi, ana tattoo ndani ya jicho lake kwenye paji la uso, katika sehemu ya uso wake, kwenye meno yake na katika shavu lake.

Lakini cha kuvutia zaidi ni kuwa sehemu nyeupe ya jicho lake imewekwa tatoo kwa kutumia wino mweusi.

Upande wa mashitaka ulisema kwamba mtuhumiwa kwa kuangalia tu uso wake uliojaa tatoo, ni ishara kwamba ni uamuzi alioufanya kitambo sana,uamuzi wa kuwa mhalifu.

Baadhi wanapenda macho yao kuwa na mwonekano wa rangi nzuri ya kupendeza 

Lakini je kwa kuweka tatoo ndani ya macho yake, alitaka kuonyesha kwamba ni mhalifu na mpenda vurugu?

Mwanamume wa kwanza aliyejaribu kujidunga wino kwenye macho yake alikuwa mtaalamu na mchoraji wa Tatoo, anayejulikana kama Luna Cobra.

Hakuwa na nia ya kufanana na mtu muovu bali lengo lake lilikuwa kufanana na viumbe vilivyokuwa kwenye filamu maarufu ya Dune.

''Wakati unapodungwa ile sindano inayoweka wino kwenye macho yako unahisi kama mtu anakudunga kisha unahisi kama mtu umewekewa mchanga ndani ya macho,'' anasema Cobra ambaye kazi yake sasa ni kurembesha watu macho na kuwabadilisha rangi za wacho yao. Anaishi nchini Canada.

Sindano moja huwa na wino wa kutosha kufunika robo ya jicho. Unahitaji zaidi ya sindano moja ya wino kubadilisha rangi ya sehemu nyupe ya jicho. Rangi hio huwa ni ya kudumu haiwezi kutoka tena.

Kylie anasema watu wamependa sana rangi ya macho yake 

Kylie Garth
Kylie ana macho ya buluu na anasema kwamba watu wengi humtizama sana kitu anachokifurahia.

Kylie anafurahishwa sana kuwa na mwonekanao wa kipekee ikizingatiwa kwamba yeye hufanya kazi katika duka ambalo hutoa huduma kwa wanaotaka kutogwa mjini Sydney Australia.

Kabla ya kuamua rangi ya wino aliotaka kutumia ndani ya macho yake, Garth aliwahi kujaribu kuweka tatoo mbali mbali ikiwemo kwenye uso wake, kutoga masikio yake na hata ulimi wake.

Jason Barnum anasema unapobadilishwa rangi ya mambo, unahisi kama mtu anakudunga kisha unahisi shinikizo flani halafu unahisi kama umemwagiwa mchanga kwenye jicho lakini hauhisi uchungu wowote. ''

 Mwanamuziki huyu alisema alihisi macho yake yalikuwa yanachomeka baada ya kufanyiwa tatoo ya jicho 

Hata hivyo mwanamuziki mmoja wa Poland anatofautiana na wanavyosema wengine. Alinaswa kwenye kanda ya video akiwekwa tatoo ndani ya jicho lake. Siku chache baadaye, alihisi kama vile jicho lake linachomeka hali iliyomzuia hata kulala.

Garth anasema kwamba macho yake yamewapendezea wengi sana.

Labda ni lile wazo tu la mtu kudungwa sindano ndani ya jicho lake ndilo linawahofisha wengi. Watu huniambia, ''eeh, siamini ulifanywa hivyo. Lakini sijawahi kusikia mtu akisema kwamba ninatisha.''

Luna Cobra hata hivyo anasema yeye huwashauri vijana kusubiri hadi wapate kazi kabla ya kuanza kujibadilisha rangi ya macho, kwa sababu huenda ikawakosesha kazi. Kile alichoanza kukifanya kama jaribio la kujifurahisha tu kwa kutaka kuwa na mwonekano wake wa kikepekee kimewavutia watu wengi sana.

Lakini madaktari wa macho walanaani kasumba hii wakisema ni hatari na inaweza hata kumfanya mtu kupofuka. 
via>>BBC 

Bonyeza hapa Tukupe habari zote mara tu Tunapozitoa "HABARI" VITUKO "MAPENZI"MAGAZETI,UDAKU>
Endapo una Habari,Picha,Video,Tangazo au Tatizo Lolote wasiliana nasi kwa namba  +255 688 405 951

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post