Jeshi
la polisi mkoa wa Morogoro limefanikiwa kudhibiti wanachi waliobeba
madumu wakitaka kuiba mafuta baada ya lori la mafuta kuanguna katika
eneo la Mikese mkoani Morogoro.
Dereva wa lori Deogras John hilo akizungumzia tuki hilo la ajali
amesema chanzo cha ajali alikuwa akijaribu kukwepa mtoto aliekua akivuka
barabara ndipo gari ikapoteza mweleko na kupinduka mara kadhaa ambapo
wananchi walijitokeza na madumu na kuanza kuiba mafuta.
Nao wananchi wa eneo la Mikese katika hali iso ya kawaida
wamelalamikia jeshi la polisi kuwazuia kuiba mafuta na kueleza kuwa
wamefanya kazi ya kumuokoa dereva kwa kumtoa kwenye gari na hivyo
walipaswa kuchukua mafuta kama ujira wao.
Endapo una Habari,Picha,Video,Tangazo au Tatizo Lolote wasiliana nasi kwa namba +255 688 405 951