Jeshi
la polisi wilayani Kahama Mkoani Shinyanga linawasaka wanawake watatu kwa
tuhuma za kuwalisha chips yenye madawa ya kulevya, madereva wawili wa roli la
mafuta kutoka Dar es Salaam kwenda nchini Rwanda.
Kamanda
wa polisi Mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha amesema tukio hilo limetokea usiku
wa kuamkia mwaka mpya katika maeneo ya Phantom mjini Kahama, baada ya madereva
hao kuokolewa asubuhi na wasamaria wema.
Kamugisha
amesema madereva hao waliwapatia Lifti wanawake watatu waliodai wanatoka
Misigri Mkoani Singida kwenda Nyakanazi Mkoani Kagera lakini walipofika
wilayani Kahama walishuka kwenda kununua chips.
Katika
tukio hilo wanawake hao baada ya kununua chips walirudii kwenye gari wakawapa
madereva hao ikiwa imefungwa kwenye mifuko, baada ya kuila walilewa wote na
wanawake hao walianza kutaka kunyonya mafuta kutoka kwenye tenki la roli hilo.
Hata
hivyo Kamugisha amesema juhudi hizo za kuiba mafuta hayo ziligonga mwamba baada
ya kushindwa kufungua mfuniko wa siri ulikuwa kwenye tenki la mafuta hayo mpaka
ilipofika asubuhi wanawake hao walitelekeza roli hilo na kutoroka pasipo
julikana.
Aidha
Kamanda kamugisha amewataja madereva hao kuwa na Birari Muhamed (49) mkazi wa
mbezi Dar es salaam pamoja na msaidizi wake Amiri Salum (20) ambaye pia ni mkazi
wa Dar es salaam, waliokuwa wakiendesha roli la mafuta namba T860 DCY aina ya
IVECO na hali zao zinaendelea vizuri baada ya kupata matibabu katika hospitali
ya mji wa Kahama.
Social Plugin